Sote tunajua tunaishi katika ulimwengu wa teknolojia. Inazidi kuwa ngumu zaidi kuweka nywila yaani password zetu kuwa siri kutoka wadukuzi maarufu kama hackers. Hackers wa kompyuta wanaonekana kuwa na uwezo wa kuingia katika kitu chochote wanachotaka na kuiba mamilioni ya pesa huku wakisababisha uharibifu wa thamani ya mabilioni ya dola. Kwa hivyo, hebu tuangalie Hackare 10 hatari zaidi ulimwenguni 1. Wa kwanza ni, Jeremy Hammond. Jeremy Hammond ni hacker aliyeiba nambari za kadi za benki 60,000 na kuzitumia kutoa michango kwa mashirika ya misaada kwa jamii 2. Wa pili ni Kevin Mitnick Kevin Mitnick ndiye hacker maarufu zaidi ulimwenguni. Mara moja alishawahi kuwa mtu aliyesakwa sana au 'most wanted' na FBI kwa sababu alidukua mashirika makubwa 40, Kevin sasa ni mshauri wa usalama anayeaminika na serikali nyingi ulimwenguni. 3. Wa tatu ni Gary McKinnon Alama iliyoachwa na Mitnick imekuja pitwa na McKinnon, hacker muingereza ambae alidai juhudi zake za udukuzi ilikuwa ni jitih...