HACKERS 10 Hatari Waliotikisa Dunia
Sote tunajua tunaishi katika ulimwengu wa teknolojia. Inazidi kuwa ngumu zaidi kuweka nywila yaani password zetu kuwa siri kutoka wadukuzi maarufu kama hackers. Hackers wa kompyuta wanaonekana kuwa na uwezo wa kuingia katika kitu chochote wanachotaka na kuiba mamilioni ya pesa huku wakisababisha uharibifu wa thamani ya mabilioni ya dola. Kwa hivyo, hebu tuangalie Hackare 10 hatari zaidi ulimwenguni
1. Wa kwanza ni, Jeremy Hammond.
Jeremy Hammond ni hacker aliyeiba nambari za kadi za benki 60,000 na kuzitumia kutoa michango kwa mashirika ya misaada kwa jamii
2. Wa pili ni Kevin Mitnick
Kevin Mitnick ndiye hacker maarufu zaidi ulimwenguni. Mara moja alishawahi kuwa mtu aliyesakwa sana au 'most wanted' na FBI kwa sababu alidukua mashirika makubwa 40, Kevin sasa ni mshauri wa usalama anayeaminika na serikali nyingi ulimwenguni.
3. Wa tatu ni Gary McKinnon
Alama iliyoachwa na Mitnick imekuja pitwa na McKinnon, hacker muingereza ambae alidai juhudi zake za udukuzi ilikuwa ni jitihada zake za kutaka uthibitisho wa uwepo wa Eliens, waasisi wa teknolojia wanadai kama asingekamatwa basi angesababisha vita kubwa sana. Mckinnon alifanikiwa kuingia kwenye kompyuta za jengo nyeti la Pentagon na kuacha ujumbe "Ulinzi wenu ni takataka".Kumbuka,Pentagon ni jengo la makao makuu ya Idara ya Ulinzi ya marekani.
4. Wa nne ni Albert Gonzalez
Kulingana na gazeti la New York Daily News, Gonzalez, alianza alianza udukuzi akiwa shule yake ya upili huko Miami. Mwishowe alikua akifanya kazi kwenye forum ya mahaka na uhalifu iitwayo Shadowcrew.com na yeye alionekana kuwa mmoja wa wasimamizi na mahaka bora wa forum hiyo
5. Wa tano ni Jeanson James Ancheta
Ancheta alikuwa mwanafunzi wa skondari huko California kabla ya kufikia uamuzi wa kuacha shule mwaka 2001. Ancheta Alifanya kazi kwenye internet cafe na kulingana na familia yake alitaka kujiunga na jeshi. Mzaliwa huyo wa California ndiye aliyekuwa haka wa kwanza kushtakiwa kwa kudhibiti mifumo iliyoendeshwa kwa kompyuta kwa code zilizojiendesha zenyewe maarufu kama bots - kutuma idadi kubwa ya spam kwenye mtandao.
6. Wa sita ni Kevin Poulsen.
Wakati mwingine hackers wanaweza kuonekana kuwa hawana hatia katika maisha yao ya kila siku. Chukua mfano, Kevin Poulsen, ambaye sasa ni Mhariri wa tovuti maarufu ya wired.com. Lakini hapo awali alikuwa haka mmoja hatari sana, Mnamo 1983, Poulsen alipokuwa na umri wa miaka 17, alinaswa akidukua mtandao wa kompyuta wa Pentagon uitwao ARPANET.
7. Wa saba ni Adrian Lamo
Kwa sababu alipendelea kuzurura katika mitaa akiwa na mkoba na mara nyingi hakuwa na mahali rasmi pa kuishi, Lamo alipewa jina la "The homeless hacker."
8. Wa nane ni Jonathan James.
Jonathan James alikuwa mtoto wa kwanza kupatikana na hatia na kufungwa jela kwa udukuzi huko marekani. Kuanzia umri wa miaka 15, alidukua Bell South, mfumo wa shule ya Miami-Dade, NASA, na Idara ya Ulinzi, na kuiba programu ilyosadikika kuwa na thamani ya dola milioni 1.7 kutoka serikali ya marekani.
9. Wa tisa ni grupu la mahaka waitwao Aurora.
Kundi hili ndio watu waliowajibika na "Operesheni Aurora", udukuzi wa kimataifa na mgumu uliofanywa mwaka 2009 ambao ulilenga kampuni 34 ikiwa ni pamoja na Google na Yahoo !. Kulingana na kampuni ya ulinzi na usalama wa mtandao iitwayo McAfee, lengo la msingi la shambulio hilo lilikuwa kupata na kubadilisha codes za kampuni hizi kubwa.
10. Wa kumi ni Robert Tappan Morris
Mmoja wa haka wa kwanza waliojulikana alikuwa Robert Tappan Morris, muundaji wa "Morris Worm" - kirusi wa kwanza wa kompyuta kwenye mtandao ambae inasemekana aliambukiza karibu kompyuta 6,000. Robert aliiachia akiwa anasomea Cornell mnamo 1988, na inaonekana alikuwa akijaribu kutathmini ukubwa wa mtandao. Kirusi huyo alibuniwa ili kukagua kila kompyuta na kujikopi mwenyewe.
Comments
Post a Comment