GAMAL NASSER: Rais Aliyeamini MABAVU Kuliko AKILI! Gamal Abdel Nasser aliongoza mapinduzi ya 1952 yaliyomng'oa madarakani Mfalme Faruk I na kumuweka Jenerali Mohamed Naguib, wakapishana kiitikadi akampindua na kukalia kiti mwenyewe kupambana na Israel badala ya kuijenga Misri na Afrika kama alivyotuamisha kipindi cha mapinduzi, mwaka 70 akafa kifo cha ghafla na kuicha Misri njia panda, wa biblia wakasema alijichanganya kuligusa taifa teule la Mungu maana imeandikwa ukiwagusa utaangamia, ukiwabariki utabarikiwa ameeenii! Enzi za Nasser Misri ilikuwa nyumbani kwa wapigania uhuru wa nchi za Afrika na kiarabu. Nakumbuka hata Saddam Hussein alipewa hifadhi Misri.Ni baada ya jaribio lake la kumpindua Generali Abdul Karim Qassim kufail. Kipindi hicho Saddam alikuwa janki wa miaka 22 tu. Rais Gamal alimpa hifadhi ya kisiasa, pesa ya kujikimu na kumpeleka Cairo University kupiga sheria. Waliosoma naye wanasema mshikaji aliingia darasani kwa manati, muda mwingi aliutumia kula fegi kwa ...