OMAR AL-BASHIR: Rais Aliyetema Mate Juu Yakamdondokea Mwenyewe

OMAR AL-BASHIR: Rais Aliyetema Mate Juu Yakamdondokea Mwenyewe Tangu Sudan ipate uhuru mwaka 1956 imekuwa ni nchi ya vuta nkuvute. Full kunyoana nywele bila maji. Waafrika wanachinjana, wachina na wazungu wanakunywa mafuta, halafu vyombo vya habari vinasema tatizo la Sudan ni ukabila wa waarabu kuwabagua weusi kwa sababu ya ukafir wao na sisi tunakubali kama nyumbu vile. Wageni wanatugombanisha kama madume ya ng’ombe kule kwa wafugaji wakati wa mashindano ya wanyama, ng'ombe wanatwangana bila kujua sababu. Akili za ngo’mbe ndo zinatusumbua Afrika. Leo Bashir ametimuliwa Ikulu kama mbwa koko wa Afande Muroto wa Dodoma na wa Sudani kutokwa machozi ya furaha ambayo siku za usoni yatageuka kuwa machozi ya damu! Muda haudanganyi! Unajua kilichomgharimu al-Bashir ni kushindwa kuusoma mchezo mapema na kuishia kuwatemea mate ndugu zake waafrika yakamrudia. Alimtimua kazi na kumtia jela Al- Tulab waliyekuwa naye tangu mapinduzi kwa sababu tu Marekani walimwambia afanye hivyo na ule mwaka wa shetani ulipofika al-Bashir naye akatupwa gereza lile lile alilomfunga jamaa yake, halafu akasema gereza lile ni hatari kwa afya ya binadamu, sasa siju al- Tulab na wenzake aliowafunga mle walikuwa mbuzi? Lakini pia siku ile Gaddafi anakufa Bashir alisema wasudan wanamshukuru Mungu kwa zawadi ya kifo cha Gaddafi na kujigamba kwamba vile vifaru, silaha na makombora yaliyotumika kummaliza Gaddafi aliyafadhili yeye kwa asilimia 100. Ntakusimulia ilikuaje, acha twende kwenye hoja kwanza!

Comments

Popular posts from this blog